Uwepo wa Mtambo wa CT Scan Hospitali ya Tosamaganga.

Hafla ya Uzinduzi wa jengo la Idara ya dharula Tosamaganga hospitali lililo zinduliwa na Muhashamu Baba Askofu Tarcisius J.M. Ngalalekumtwa wa jimbo la Iringa iliyofanyika mnano tarehe 12/5/2023.
Uongozi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa Tosamaganga, inawakaribisha Wananchi wote wa Mkoa wa Iringa kwenye kambi kubwa ya bure ya upasuaji wa kurekebisha viungo. Itakayoanza siku ya Juma Tatu Tarehe 16 February hadi Tarehe 28 February mwaka 2025.
Maboresho hayo makubwa yanafanywa kwa kutumia mapato ya ndani lakini pia jengo la I.C.U linajengwa kwa Michango iliyopatikana kwa Mbio za hisani za kuchangia I.C.U zilizofanyika tarehe 22 mwezi Jun mwaka 2023. hata hivyo bado kuna uhitaji wa wadau wa Afya na mashirika mbalimbali kuombwa kuchangia ujenzi wa I.C.U kwani bado hatujafikia Malengo.
Mkurugenzi mkuu wa Hospitali ya Rufaa ngazi ya mkoa Tosamaganga, anawaalika wananchi wote wa ndani na nje ya Mkoa wa iringa siku ya Tarehe 27 Mwezi wa Tisa katika kambi ya upasuaji wa madaktari bingwa wa kurekebisha viungo kutoka Ujerumani. Kambi hii ni ya bure hivyo basi wakazi wote wa Iringa na Vitongoji vyake mnakarishwa…