Ujio wa Madaktari Bingwa Kutoka Ujerumani.

Uongozi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa Tosamaganga, inawakaribisha Wananchi wote wa Mkoa wa Iringa kwenye kambi kubwa ya bure ya upasuaji wa kurekebisha viungo. Itakayoanza siku ya Juma Tatu Tarehe 16 February hadi Tarehe 28 February mwaka 2025.
Pichani ni Mtaalamu wa CT- SCAN Sr. Astrida akitoa maelezo mbele ya kamati ya siasa ya Mkoa wa Iringa Ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa kwanza upande wa kushoto Ndugu Daud Yassin akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Halima Dendego wa pili kutoka upande wa kushoto na viongozi wengine walipotembelea Hospitali…
Maboresho hayo makubwa yanafanywa kwa kutumia mapato ya ndani lakini pia jengo la I.C.U linajengwa kwa Michango iliyopatikana kwa Mbio za hisani za kuchangia I.C.U zilizofanyika tarehe 22 mwezi Jun mwaka 2023. hata hivyo bado kuna uhitaji wa wadau wa Afya na mashirika mbalimbali kuombwa kuchangia ujenzi wa I.C.U kwani bado hatujafikia Malengo.