Timu ya Madaktari kutoka Ujerumani wakiendelea na Majukumu katika zoezi la kufanya Upasuaji wa kurekebisha Viungo.




Uongozi wa Hospitali ya Tosamaganga Unawataarifu Wakazi wa mkoa wa Iringa na Watanzania wote kwa ujumla kuwa Kutakua na Ujio wa Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Kurekebisha Viungo Kutoka Ujerumani , Watakuepo Hospitali ya Tosamaganga Kuanzia Tarehe 17-27 Mwezi wa 10-2023 Wote Mnakaribishwa kupata Matibabu ya Kibingwa bure.
Hafla ya Uzinduzi wa jengo la Idara ya dharula Tosamaganga hospitali lililo zinduliwa na Muhashamu Baba Askofu Tarcisius J.M. Ngalalekumtwa wa jimbo la Iringa iliyofanyika mnano tarehe 12/5/2023.
Maboresho hayo makubwa yanafanywa kwa kutumia mapato ya ndani lakini pia jengo la I.C.U linajengwa kwa Michango iliyopatikana kwa Mbio za hisani za kuchangia I.C.U zilizofanyika tarehe 22 mwezi Jun mwaka 2023. hata hivyo bado kuna uhitaji wa wadau wa Afya na mashirika mbalimbali kuombwa kuchangia ujenzi wa I.C.U kwani bado hatujafikia Malengo.