Salamu ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kutoka Tosamaganga Regional Referral Hospital

Katika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani, uongozi wa Tosamaganga Regional Referral Hospital (TRRH) unapenda kutoa salamu za dhati kwa wafanyakazi wote wanaojitolea kila siku kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kwa jamii.
Wafanyakazi wa hospitali yetu ndio nguzo kuu ya mafanikio yetu. Kupitia kujituma, weledi, na moyo wa huduma, mmeendelea kuleta matumaini kwa wagonjwa na familia zao. Kila siku mnachangia kwa kiwango kikubwa katika kuboresha maisha ya watu na kuimarisha sekta ya afya.
Licha ya changamoto zinazoweza kujitokeza katika utoaji wa huduma, mmeendelea kuonesha uthabiti, mshikamano, na kujitoa kwa hali ya juu. Hii ni ishara ya uzalendo na dhamira ya kweli ya kuwahudumia wananchi.
Tunawapongeza sana kwa kazi kubwa mnayoifanya. Tunathamini mchango wenu na tunaahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kazi ili muweze kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi zaidi.
Kwa niaba ya uongozi, tunawatakia heri njema katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
P.d Dkt. Benjamin C. Mfaume
Mkurugezi Mkuu
Tosamaganga Regional Referral Hospital (TRRH)
